NKupamah media:
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa filamu waliopata Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) nchini Nigeria leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia waliokaa ni Msanii Single Mtambalike (Richie Richie) ambaye ndiye mshindi wa kwanza kwa Filamu za Kishwahili barani Africa, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa filamu waliopata Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) leo jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah ,Mwambene (kushoto) na kulia ni Single Mtambalike (Richie Richie) ambaye ndiye mshindi wa kwanza kwa Filamu za Kiswahili barani Africa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba.
Msanii Single Mtambalike (Richie Richie) ambaye ndiye mshindi wa kwanza kwa Filamu za Kiswahili barani Africa akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa Filamu walioiwakilisha nchi katika mashindano ya Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFFA) Simon Mwakifamba na Msanii wa Kitanzania anayeishi Marekani Honey Moon.Hafla hiyo imeambatana na kukabidhiwa vyeti vyapongezi kutoka Serikalini.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah ,Mwambene akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii wa filamu waliopata Tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA) nchini Nigeria leo jijini Dar es Salaam.Ambapo wasanii hao walikabidhiwa Vyeti vya pongezi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango wao katika kukuza tasnia hiyo hapa nchini.
WAFAMASIA WA BODI YA CHAKULA DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO JUU YA UDHIBITI WA DAWA.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa Zanzibar Zaharani Ali Hamad akifungua mafunzo ya siku tano ya udhibiti wa Dawa kwa wafamasia wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar katika Ukumbi wa Ofisi za Malaria Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
Mrajis wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar ambae pia alikuwa mwenyekiti katika mafunzo hayo Dk. Burhani Othman Simai akiongoza mafunzo hayo.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa Dawa Nasir Salum Buheti akiuliza swali na kutoa mchango wake katika mafunzo ya udhibiti wa Dawa.
Mkufunzi wa Usajili wa Dawa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) David Robert Matle akitoa mada kusu njia bora za Uagiziaji na udhibiti wa Dawa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar.
Picha ya pamoja ya washiriki wa Mafunzo ya siku tano ya udhibiti wa Dawa, yaliyoandaliwa na Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
……………………………………………………………………….
Na Fatma Kassim
BODI ya Chakula Dawa na Vipodozi inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa Dawa zinazoingia nchini ni salama na zinafaa kwa matumizi ya mwanadamu.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zahran Ali Hamad wakati akifungua mkutano wa siku tano wa udhibiti wa dawa kwa wafamasia wa hapa nchini.
Amesema ni vyema wafamasia hao kutumia taaluma walinayo ili kuhakikisha wanadhibiti uingiaji wa dawa zisizo na viwango kwa lengo la kumkinga watumiaji na maradhi mbali mabali yanayotokana na dawa.
Amewataka wafamasia hao kuongeza jitihada katika suala zima la udhibiti wa dawa wakati zinapoingia nchini kwa kuwezesha kuepuka matatizo ya afya za wanaadamu.
Alisema hivi sasa Tanzania ni miongoni mwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni vyema kuongeza ushindani wa utoaji wa huduma bora kwa jamii na kuhakikisha kuwa Zanzibar haiingizi dawa bandia.
Mrajis wa Bodi ya Chakula Dawa na vipodozi Dk Burhan Othman Simai amesema kuwa katika mpango mkakati wao ni kuwapatia mafunzo wafanyakazi wake ili kuweza kukabilina na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni
Amefahamisha kuwa katika kukabilina na hali iliyopo hivi sasa ni vyema Serikali kuongeza wafanyakazi wa kada ya ufamasia ili kuweza kufanyakazi kwa ufanisi katika sehemu tofauti.
Alisema wataendeleza mafunzo kwa wafanyakazi wake ili kwenda sambamba na haja iliyopo na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mapema mkufunzi wa usajili wa Dawa kutoka Mamlaka ya Chakula Tanzania David Robert Matle amesema ni vyema dawa kuifanyia usajili kwa kutimiza vigezo vya ubora, usalama wa dawa hizo.
Amesema lengo la usajili wa dawa ni kuwalinda wanaadamu wasipate madhara yanayotokana na dawa.


0 comments :
Post a Comment