RC Makonda Aitisha Kikao na Walimu ili Kujadili Matatizo Yanayowakabili


Mkuu  wa Mkoa  wa  Dar  es  Salaam  Paulo  Makonda  amemwagiza Ofisa Elimu,Raymond  Mapunda  kuitisha  mkutano  wa  walimu  March 26 mwaka  huu ili  kujadili matatizo  yanayowakabili likiwemo  la  kutopanda  madaraja  kwa  wakati.

Makonda  aliyasema  hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akikabidhi  madawati 500 katika shule  ya  msingi  Kawawa yaliyotolewa  na  kampuni  ya  simu  za  mkononi  ya  Tigo.

Mkuu huyo alieleza kuwa yapo matatizo mengi  yanayowakabili walimu yanayotokana  na  watu  wanaojinufaisha matumbo  yao kwa kuwalipa walimu hewa

Katika hatua nyingine,Makonda aliwataka walimu kutovunjwa moyo kutokana na matatizo yaliyopo katika sekta  ya  Elimu.

Naye mkurugenzi wa kampuni ya Tigo,Diego Gutierrez alisema kuwa mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni ya Tigo kuunga mkono jitihada za serikali katika kuleta  maendeleo ya elimu nchini

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment