Sergei
Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema leo Jumatatu kuwa
uingiliaji kijeshi huko Libya unawezekana iwapo tu Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa litaidhinisha suala hilo.
Lavrov
ameyasema hayo baada ya mazungumzo yake na Waziri mwenzake wa Tunisia
huko Moscow kama ninavyomnukuu” tunafahamu kuhusu mipango ya uingiliaji
kijeshi, ikiwemo hali ya mambo huko Libya. Mtazamo wetu wa pamoja ni huu
kwamba uingiliaji huo unawezekana tu kwa kibali cha Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa,” mwisho wa kumnukuu.
Waziri wa
Mambo ya Nje wa Russia amesema oparesheni yoyote inayoweza kutekelezwa
dhidi ya magaidi huko Libya ni lazima ibainishwe bila ya utata ili
kuzuia tafsiri za uwongo na zenye kupotosha.(VICTOR)


0 comments :
Post a Comment