WACHEZAJI WA MPIRA WA MAGONGO WATAKIWA KUJITUMA ILI KUILETEA SIFA NCHI.

Nkupamah media: 

NPE1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwa na timu ya wachezaji wa mchozo wa Magongo Hokkey.
………………………………………………………………………………………………..
Na. Najaha Bakari
Wachezaji wa mpira wa Magongo (Twende Hockey) wametakiwa kujituma  na kuiletea sifa nchi katika mashindano yao ya kufuzu kombe la Afrika yanayotarajia kufanyika  Machi 18 hadi 28 mwaka huu nchini Namibia.
Rai hiyo imetolewa  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye  wakati wa kukabidhi bendera kwa  timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
“Nawatakia mafanikio katika mashindano hayo, muwe na moyo wa kushinda siyo kushiriki, na nawaahidi kuwapokea mkirudi na ushindi“alisema Mhe. Nnauye”.
Aidha, Mhe. Nnauye amesema kuwa Serikali itakuwa karibu na Vyama/Mashirikisho ya michezo ili kuhakikisha kuwa michezo yote inafanya vizuri  kwa lengo la  kuitangaza na kuiletea sifa nchi yetu.
Waziri Nnauye aliwaomba  NMB na wadhamini wengine kusaini mikataba ya muda mrefu kwani matokeo mazuri hupatikana kwa kuwekeza kwa muda, vilevile  aliwataka wadhamini kudhamini michezo yote na siyo soka pekee.
Kwa upande wake Afisa fedha Mkuu kutoka NMB Bw. Waziri Barnabas alisema kuwa NMB imekuwa ikidhamini mchezo huo kwa miaka miwili sasa na michezo mingine, ambapo  aliwataka wanamichezo kuwa na ari ya kuleta ushindi na sifa kwa Taifa  kuwafanya wadhamini kuwa na moyo wa kudhamini zaidi.
Awali Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo Bw. Abraham Sykes, alisema mchezo huo ulisahaulika ila anaamini kuwa vijana wake wameandaliwa vyema hivyo watafanya na wataendelea kufanya vizuri.
Timu ya Mpira wa Magongo inatarajia kuondoka nchini tarehe 13 Machi mwaka huu kuelekea nchini Namibia kwa mashindano hayo, ambapo NMB wamewakabidhi hundi ya Sh.milioni 25 na mabegi ya kuweka vifaa vya mchezo huo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment