Wafanyakazi 800 wakopeshwa bilioni 1.2 kwa ajili ya kusoma

Nkupamah media:
unnamed
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa Mifuko ya hifadhi ya jamii imekua chachu ya maendeleo ya taifa kutokana na uwekezaji unaofanywa na mifuko hiyo pamoja na mikopo mbalimbali inayotolewa kwa wanachama kujikwamua kimaisha.
………………………………………………………………………………………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Arusha,Mfuko wa Pensheni wa LAPF , umetoa mkopo wa sh 1.2 bilioni  kwa watumishi 800   ambao ni wanachama wa mfuko huo katika kipindi cha mwaka 2015/16 ili wajiendeleze kielimu.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa mfuko huo, James Mlowe alitoa taarifa hiyo jana, wakati akizungumza na waandishi juu ya  mkutano mkuu wa mwaka wa mfuko huo ambao unatarajiwa kufanyika jiji hapa kuanzia Machi 10 mwaka huu.
Mlowe alisema, mfuko huo ulizindua fao hilo la elimu mwaka jana  ambalo sasa limekuwa na manufaa makubwa kwa watumishi ambao wanataka kujiendeleza.
Alisema sambamba na fao hilo, katika mkutano mkuu wa saba ya mwaka huu, mfuko huo unatarajia kuzindua utaratibu wa maisha popote na LAPF ikiwa ni mikakati ya mfuko huo kupanua huduma.
Akizungumzia hali ya mfuko huo, mkuu wa kitengo cha tathmini ya mfuko , Abubakar Ndwata alisema hadi sasa mfuko una wanachama 156,000 na ukiwa na thamani ya Sh1.087.Trilioni
Alisema makusanyo kwa mwaka  uliopita ni sh 203 bilioni ambapo malipo kwa mwaka jana ilikuwa ni Sh 88 bilioni.
Akizungumzia mkutano  alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa, George Simbachawene.
Alisema katika mkutano huo, mada mbali mbali zitatolewa ikiwepo  taarifa ya mfuko, taarifa ya fedha, mipango ya uwekezaji na ugonjwa wa Tezi dume.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment