Timu
za Tanzania zinazoshiriki michuano ya Kimtaifa kwa ngazi ya vilabu
ikiwemo Azam na Yanga katika michezo yao leo Macho 12.2016 zimeweza
kuchomoka na ushindi ugenini hali ambayo zinajiweka katika nafasi nzuri
ya kusonga mbele zaidi kwenye michuano hiyo.
Yanga
wao wamweza kuchomoka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya wapinzani wao,
Warwanda, Klabu ya APRA ambayo ni ya Jeshi. Kwa upande wa Azam wao
wamepata ushindi huo usiku huu baada ya kuifunga bao 3-0 dhidi ya
wapinzani wao Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kombe la
shirikisho ikiwa ni saa chache baada ya Yanga kupata ushindi huo wa
magoli 2-1 dhidi ya APR Kigali, Rwanda.
Azam
walipata bao la kwanza lilifungwa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika
ya 50 baada ya kuachia shuti kali nje ya 18 kufuatia kona iliyopigwa na
Ramadhani Singano ‘Messi’ kuokolewa vibaya na mabeki wa Wits kisha mpira
kumkuta Sure Boy.
Dakika
ya 57 baadaye, beki wa pembeni wa Azam FC Shomari Kapombe aliipatia
Azam bao la pili baada ya mabeki wa Wits kufanya uzembe kuokoa mpira
kisha Kapombe akaserereka na kupiga mpira uliotinga moja kwa moja kwenye
kamba za Wits.
John Bocco ‘Adebayor’
alihitimisha kipigo hicho kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 60 na
kuiweka Azam kwenye mazingira ya kusonga mbele mbele kwenye michuano
hiyo.


0 comments :
Post a Comment