Machar alikuwa katika makao makuu ya waasi yaliyo katika mji wa Pagak
Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar, amerejea nchini humo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili kama sehemu ya utekelezwaji wa mkataba wa amani.
Atakapowasili mjini Juba, Bwana Machar anatarajiwa kuchukua wadhfa wake wa makamu wa rais.
Msemaji wake amethibitisha kwamba bwana Machar alikuwa katika makao makuu ya waasi yaliyo katika mji wa Pagak mpakani na taifa jirani la Ethiopia.
Baadhi ya waasi tayari wamewasili mjini Juba, na akizungumza punde baada ya kuwasili, naibu kiongozi wa waasi Alfred Ladu Gol amesema wakati umewadia kwa raia wote wa taifa hilo kuungana na kufanya kazi kwa pamoja.BBC
0 comments :
Post a Comment