Naibu Waziri Ofisi ya Wazikri
Mkuu (watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akifafanua jambo
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kanzidata ya watu wenye
ulemavu katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 11, 2016
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu (watu wenye Ulemavu)Mhe. Dkt. Abdallah Possi akifuatilia
uwasilishwaji wa takwimu za Watu wenye Ulemavu kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk.Albina Chuwa wakati wa Uzinduzi wa
kanzi data hiyo Aprili 11, 2016 Dar es Salaam
Mwenyekiti wa wasioona Bw. Luis
Benedicto akichangia hoja wakati wa Uzinduzi wa Kanzidata ya watu wenye
ulemavu katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 11,
2016
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu Dk.Albina Chuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari
kuhusu Kanzidata mara baada ya uzinduzi wa kanzidata hiyo ya watu wenye
ulemavu katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 11 2016,
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye ulemavu) Dkt. Abdallah Possi amezindua rasmi kanzidata ya
watu wenye ulemavu, ambayo itasaidia katika upatikanaji wa taarifa
zinazohusiana na watu wenye ulemavu nchini na kuwawezesha wadau wengine
katika kuboresha sera na programu zinazolenga kuboresha maisha ya watu
wenye ulemavu nchini.
Akizungumza mara baada ya
uzinduzi wa kanzidata hiyo Katika Ofisi ya Waziri Mkuu leo Jijini Dar es
Salaam, Dkt Abdallah Possi amesema kanzi data hiyo itakayotumika kutoa
takwimu ya watu wenye ulemavu nchini iwe ni fursa ya kuwasaidia watu
wenye ulemavu kwa, kujikwamua kiuchumi na kuondokana na unyanyapa
unaofanywa na baadhi ya watu.
“Ni matarajio yangu kwamba
kanzidata hii itasaidia mambo kadhaa muhimu, kubwa zaidi ni upatikanaji
wa taarifa katika mfumo rafiki utakaosaidia watumiaji kufanya uchambuzi
wa kina zaidi kulingana na mahitaji yao yatakayosaidia kuleta uelewa kwa
watu kuhusu ulemavu kwa ujumla na umuhimu wa kuhusisha mahitaji ya watu
wenye ulemavu kwa ajili ya maendeleo endelevu” alisema Dkt. Possi.
Aidha Mkurugenzi wa Ofisi ya
Takwimu ya Taifa (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa wajibu wa Ofisi ya
Takwimu ya Taifa ni kutunza na kutoa kumbukumbu kwa ajili ya makundi
mbalimbali na katika kufanikisha hilo ameomba ushirikiano kutoka chama
cha watu wenye ulemavu na mashirikisho yake ili kuboresha kanzidata hii
ya watu wenye ulemavu.
Dkt. Chuwa alisisitiza kuwa, ili
kanzidata hii iweze kufanya kazi kwa urahisi inahitaji ushirikiano
kutoka Sekta binafsi ili kuwezesha kukamilisha andiko lililoko katika
hatua za mwisho za ukamilishaji wa kanzidata na kwa kuanzia kanzidata
hiyo imeanza kwa majaribio katika Wilaya ya Bagamoyo.
Kanzidata hii imetayarishwa na
Ofisi ya Takwimu ya Taifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa na
dhumuni la kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa urahisi na ufuatilia
wa takwimu ya masuala ya Watu wenye Ulemavu.
0 comments :
Post a Comment