Serikali ya Marekani imeihakikishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendeleza uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili ikiwa pamoja na kutoa ufadhili na misaada mbalimbali ya miradi ya maendeleo hasa katika sekta za afya na Elimu.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini aliyeongozana na Ujumbe wa watu 15 wanaoshughulikia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani hapa nchini Waziri wa Mambo ya Nje,Afrika Mashariki,Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa Dr Augustine Mahiga amsema kuwa licha ya kutokea kutoelewana kwa Serikali hiyo na Tanzania hivi karibuni lakini Nchi hiyo imsema kuwa haitasitisha kuendeleza miradi muhimu kama vile miradi ya Elimu na Afya iliyoanzishwa hapa nchini na Seikali ya Marekani sambasamba na kuendeleza Ushirikiano huo katika nyanja zingine za kimaendeleo.
Aidha Waziri Dr Mahiga amewatoa hofu watanzania na kusema kuwa miradi yote ambayo ilianzishwa hapa nchini kwa ufadhili wa Serikali ya Tanzania itaendelezwa kama ilivyopangwa hapo awali na kuahidi miradi mingine zaidi itakayoleta tija kwa Taifa sambamba na kuleta ajira kwa Watanzania walio wengi.
Kwa Upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Mark Childress amsema kuwa upo umuhimu wq kuendeleza mahusiano kati ya Tanzania na Marekani hasa katika utoaji wa misaada mbalimbali ya kimaendeleo hivyo Serikali ya nchi hiyo itaendeleza na kukuza mahusiano hayo licha ya changamoto mbalimbali za kisiasa zilipo nchini.
Nchi hiyo ya Marekani imeahidi kuongeza miradi mingi zaidi nchini itaka itakayolenga kukuza uchumi wa Tanzania na kuitoa nchi hiyo katika hali ya umasikini iliyopo hivi sasa.
0 comments :
Post a Comment