Ndugu waandishi wa Habari, wanaharakati na watanzania wote.
Chama
cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na
Uhalifu Tanzania (OJADACT). Tunalaani vikali kuzuiwa kwa Waandishi
kuingia Bungeni kwa lengo la kufanya coverage ya vikao vya Bunge la
kujadili mpango wa maendeleo ya miaka mitano na bajeti ya serikali.
OJADACT,
hatukubaliani na utaratibu wa sasa wa kutumia idara ya habari na
maelezo ya Bunge, kuwa ndio wenye jukumu la kukusanya taarifa na
kuzigawa kwa waandishi.
Ni ukweli usiopingika kuwa, maamuzi hayo yana athari zifuatazo.
Kuminya
uhuru wa haki ya kupata taarifa kwa wananchi km ilivyoainishwa kwenye
katiba ya Jamhuri ya Muungano.wa.Tanzania ibara ya 18.
Kuminya uhuru wa vyombo vya habari, ambao umekuwa ukikosa haki ya msingi iliyokosekana kwenye Katiba.
MSIMAMO WETU.
1: Kwa kuwa Bunge halioni umuhimu
wa waandishi Bingeni basi tunaviomba vyombo vyote vya habari vya binafsi
kuwatoa waandishi wao bungeni.
Tunaviomba vyombo vyote vya habari vya binafsi kususia kuandika habari za bunge hadi hapo litakapotengua utaratibu huo.
Waziri mwenye dhamana ya habari afute kauli yake ya kejeli kuwa wanaopinga utaratibu huo eti waende Mahakamani.
Ahsanteni sana wanahabari kwa kuotokia wito wetu.
Edwin Soko
Mwenyekiti (Pichani).


0 comments :
Post a Comment