Chama cha Mapinduzi kimewataka watanzania kupuuza kauli za baadhi ya wanasiasa zinazodai kuwa rais Magufuli analengo la kuwakomoa wafanyabiashara na kinazieleza kauli hizo kuwa ni za uchochezi kwakuwa serikali ya awamu ya tano haina tatizo na wafanyabiashara na watumishi waadilifu bali wanaolihujumu taifa kwa manufaaa binafsi.
Kauli hiyo ya chama imetolewa na msemaji mkuu wa CCM Christopher Ole Sendeka wilayani Simanjiro alipokuwa akizungumza na wananchi wanachama wafuasi wa CCM na viongozi wa mila katika kata ya Shambarai.
Kwa
upande katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Shabani Mdoe amewataka
wananchi kuwa makini na viongozi wasio waadilifu huku mkuu wa wilaya ya
Simaniro Mahamoud Kambona akiwata viongozi wa mila kushirikiana na
serikali katika kuleta maendeleo.
Katika
mkutano huo viongozi wa mila kutoka jamii ya wafugaji pia walipata
nafasi ya kupaza sauti na kutaka serikali na jamii iheshimu maamuzi
wanayoyatoa kama viongozi katika jamii.



0 comments :
Post a Comment