Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais IKULU, Gerson Msigwa amethibitisha Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
Mabadiliko ambayo yamefanywa ni Dk. Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Prof. Palamagamba Kabudi akichukua nafasi ya Dk. Mwakyembe na kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Msigwa amesema Dk. Mwakyembe na Prof. Kabudi wataapishwa kesho mchana Ikulu, Dar.
Zaidi waweza msikiliza Gerson Msigwa hapa chini wakati akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Clouds.
0 comments :
Post a Comment