Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimuapisha Nd,Salmin Amour Abdalla kuwa Naibu Katibu wa Baraza la
Mapinduzi katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Washauri
wa Rais wa Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla
ya kuapishwa kwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali Serikali ya Mapinduzi
leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimuapisha Nd,Asaa Ahmada Rashid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili
ya Viongozi wa Umma katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi,Raya Issa Msellem kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Baadhi
ya Viongozi mbali mbali Serikali na wananchi waliohuria katika hafla ya
kiapo kwa Watendaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi
katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw, Mzee Ali Haji kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimuapisha Bi,Mwanahija Almasi Ali kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali
katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Baadhi
ya Viongozi mbali mbali Serikali na Wananchi waliohudhuria katika hafla
ya kiapo kwa Watendaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi
katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi walipoapishwa na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Alo MOhamed
Shein,[Picha na Ikulu.]
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 30.4.2016
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein leo amewapisha viongozi mbali mbali kushika nyadhifa katika
taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Walioapishwa
ni Salmin Amour Abdallah kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Asaa
Ahmad Rashid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma,
Raya Issa Msellem kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mzee
Ali Haji kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwanahija Almasi Ali
kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hafla
ya kuwaapisha viongozi hao ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na
kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Miongoni
mwao ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun
Ali Suleiman, Waziri wa Fedha na Mipango Khalid Salum Mohammed, Waziri
wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma.
Wengine
ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi
na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu
wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Khamis Haji, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,
Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa
Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.










0 comments :
Post a Comment