KINSHASA, CONGO: Mwili wa mwimbaji nguli wa muziki wa dansi nchini DR Congo, Papa Wemba, unatarajiwa kuzikwa leo katika kijiji chaa Molokai kama kawaida kufuatia kuomba hivyo kwa ndugu na jamaa wa wanamuziki huyo hapo awali.
Tayari upande wa Serikali na kamati ya mazishi ya msanii huyo iliweza kutoa siku tatu za maombelezo na kuaga kwa ndugu na jamaa ambapo pia Serikali ya Nchi hiyo kupitia kwa Rais wake Joseph Kabila aliweza kumtunukia tuzo ya heshima ya juu katika nchi pamoja na kutoa siku tatu za maombelezo ambayo ilianza juzi na leo hii kutakuwa na maziko rasmi.
Papa Wemba alifariki hivi karibuni jijini Abidjan nchini Ivory Coast ambapo awali alipoteza fahamu akiwa jukwaani alipokuwa akitumbuiza baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali.
papa-wembaMwili wa Papa Wemba ukiwa kwenye jeneza wakati wa kuagwa. Mwili huo umewekwa katika viunga vya Bunge la DR Congo na viongozi na watu mbalimbali wamepata kutoa heshima zao za mwisho kabla ya mazisho yake hii leo.