May 27 2016, aliyekuwa mgombea Urais mwaka jana kwa tiketi ya Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan hapa nchini, Masahau Yoshida.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Lowassa ameandika; "Nimekutana na rafiki yetu Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida, nikiwa pamoja na viongozi wote wa wilaya yetu ya Monduli.

"Mbali ya kumshukuru Balozi Yoshida kwa misaada mbalimbali wanayoitoa ila zaidi tulijadiliana jinsi gani ya kufanya muendelezo na mikakati ya kuchukulia misaada hii kama nyezo za kufikia malengo ya maendeleo na sio njia ya utegemezi kiuchumi"- Lowassa

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment