Nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid na Manchester City ilichezwa usiku wa Jumatano ambapo Real Madrid ilipata nafasi ya kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila, goli ambalo limewapa nafasi ya kufuzu fainali ya mabingwa hayo.
Goli pekee la Real Madrid katika mchezo huo lilipatikana baada ya kiungo wa Manchester City, Fernando kujifunga katika dakika ya 20 baada ya Gareth Bale kupiga mpira ambao ulimgonga na kuelekea golini.
Baada ya matokeo hayo sasa Real Madrid imefuzu kucheza fainali na wapinzani wao kutoka mji mmoja, Atletico Madrid.