Mkoa
wa Kigoma umekaukiwa na sukari kuanzania Ijumaa Mei 20, 2016 na taarifa
ya Ofisi ya Biashara ya Mkoa, imesema, Wakazi wa Manispaa ya Kigoma
–Ujiji wavumilie hadi mwisho wa mwezi huu wa Mei.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani humo, kabla ya siku ya Ijumaa, sukari iliuzwa kwa bei ya shilingi elfu 5,000 kwa kilo, kwenye eneo la Manispaa ya Kigoma-Ujiji, lakini Ijumaa maeneo yote ya manispaa hiyo hayakuwa na sukari hata hiyo ya shilingi elfu 5.
Akizungumzia
uhaba huo mkubwa wa sukari mkoani humo, Afisa biashara wa mkoa wa
Kigoma Deogratius Sanga, amekiri kuwepo kwa uhaba huo na kuwataka
wananchi wa Manispaa hiyo kwua wavumilivu wakati serikali ya mkoa
inatafutia ufumbuzi tatizo hilo.
“Taarifa
toka bodi ya sukari ni kwamba ile sukari iliyoahidiwa na waziri mkuu
itafika mwisho wa mwezi huu, na tunategemea kuanzia mwezi ujao tatizo
hili litakwisha”.alisema Sanga.
Blogger Comment
Facebook Comment