Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John P. Magufuli jana
alitengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles
Kitwanga kufuatia kitendo cha waziri huyo kuingia bungeni na kujibu
swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.
Jana, Kitwanga alijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema),
Devotha Minja lililosomwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti Maalumu
(Chadema), Suzan Kiwanga na maswali na majibu yake yalikuwa kama
ifuatavyo:
Suzan: “Miaka 55 Wilaya ya Kilombero polisi hawana
nyumba wamepanga na Jimbo la Mlimba wanaishi kwenye nyumba za Tazara.
Tuwape miaka mingapi mjenge nyumba na vituo vya polisi?
Kitwanga:
Kwani wewe una miaka mingapi? Usiulize miaka ya kujenga nyumba za polisi
na vituo. Amini tutajenga tu. Halafu wewe ni rafiki yangu lazima
nikujibu hivyo.”
Suzan: Waziri unajibu kwa mapozi sana (kicheko
bungeni). Huku Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe
akionekana kucheka zaidi.
==>Hapa chini kuna Video ya dakika 7 ikimuonyesha Waziri huyo akijibu swali huku amelewa
Blogger Comment
Facebook Comment