Mtandao Wa Sky One Unawatakia Watu wote Ulimwenguni Sikukuu Na Maadhimisho Mema Ya Mei mosi 2016




Wapenzi Wasomaji wa mtandao wa Sky one blog  tunapenda kuwatakia Maadhimisho Mema ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yanayofanyika kila tarehe Moja Mwezi wa Tano (Mei Mosi) kote duniani ambayo kwa mwaka huu Kitaifa inafanyika Mkoani Dodoma kwenye viwanja vya Jamhuri-Dodoma.
Tunaamini wasomaji wetu na wadau wetu siku hii ni muhimu sana kwa wafanyakazi wetu wote hivyo ni siku ya kujitasmini namna ya ufanyaji kazi zetu. Hii pia ni namna gani ya kuona thamani ya wafanyakazi wa Nchi hii wanavyoweza kupata nafasi ya kusheherekea siku hii muhimu ambayo inatokea mara moja tu kwa kila mwaka.
Maadhimisho haya hufanyika ili kutathimini mchango, mafanikio na changamoto zinazowakabiri wafanyakati katika sekta mbalimbali ambapo wale waliotekeleza vyema majukumu yao, hupongezwa kwa kupewa zawadi ili kuongeza chachu ya utendaji kazi kwa wafanyakazi wengine huku changamoto zinazowakabiri wafanyakazi ikiwemo mishahara duni, zikielezwa bayana ili kutafutiwa ufumbuzi. 
Kitaifa hapa nchini, Maadhimisho haya yanafanyika Mkoani Dodoma, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.
Ahsanten sana Kwa ushirikiano mnaotoa kwa mtandao huu Nawatakia mapumziko mema na Mafanikio zaidi katika shughuli zenu.
Mmiliki Wa mtandao wa Sky one 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment