TAASISI
ya ushauri wa mambo ya Habari ijulikanayo kama CZI, imetoa utafiti
unaoonyesha kuwa katika kipindi cha miezi 8 ya utawala wa Rais Dkt. John
Pombe Magufuli, Watanzania wengiwanamkubali Rais na wanayo imani kubwa
Tanzania itarudi kwenye “mstari’.
Watafiti
hao, ambao ni David Saile Manoti ambaye amebobea kwenye masuala ya
Sheria, Juma George Chikawe, yeye ni mtaalamu wa Teknohama, na Dotto
Nyirenda ambaye amebobea kwenye masuala ya Kidiplomasia, wamesma
sambambana utafiti huo pia wameelezea kuwa Rais Magufuli atakapopewa
dhamana ya kukiongoza Chama Cha Mapinduzi CCM hapo Julai 27 kwenye
mkutano mkuu maalum wa chama hicho tawala, ufanisi wake katika kuongoza
nchi utaongezeka.
Kwa
mujibu wa wanazuoni hao, walisema utafiti wao ulifanyika nchi nzima na
walitumia njia ya kuwahoji watu papo kwa hapo, kuwahoji kwa kupitia simu
au kuwahoji kimakundi.
Akizungumzia
utafiti wa miezi 8 ya Rais Magufuli akiwa madarakani, Mwanasheria David
Saile Manoti, alisema, kundi la kwanza walilolihoji ni lile la vijana
wenye umri kati ya miaka 14-18 ambao wengi wao ni wanafunzi. “Baada ya
kundi hili kuhojiwa lilionyesha imani kubwa ya Rais kuleta mageuzi
makubwa ya kiuchumi, atarejesha nidhamu ya masomo mashuleni.” Alsiema
Manoti.
Mwanasheria
msomi, kutoka taasisi huru inayojishughulisha na ushauri wa mambo ya
habari, (CZI), David Saile Manoti, (katikati), akiwa na wasomi wenzake,
Bi Dotto Nyirenda, (kushoto) na Juma George Chikawe, akizungumza kwenye
mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016.
Wanazuoni hao ambao ni wanachama wa CCM, wamesema utafiti unaonyesha
Watanzania wengi wanaimani kubwa na Rais Magufuli katika mageuzi yake ya
uchumi na nidhamu.
Kuhusu
kundi la vijana wa miaka 10-30 asilimia 82 ya waliohojiwa wameonyesha
Imani kuwa Rais John Magufuli ataleta mageuzi kwenye elimu hususan
masuala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na kumaliza tatizo
la mabweni kwa wanafunzi.
Akizungumzia kundi la miaka 30-60, Manoti alisema, Watumishi wa umma wameonyesha imani kuwa
Rais Magufuli atarejesha imani kwa serikali kutokana na jinsi anavyoshughulikia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.
Aidha
utafiti unaonyesha kuwa asilimia 89.0 ya kundi hili limeonyesha imani
kubwa kwa Rais kumaliza matatizo ya wazee kwa kuanza kuwalipa posho kwa
mwezi.
Katika
utafiti huu, Manoti amebainisha kuwa umoja na mshikamano mongoni mwa
Watanzania utaimarika zaidi, vile vile kundi hili limesema Rais Magufulu
anazidi kuwa maarufu huku wapinzani wakionekana kupoteza umaarufu
klutokana na kushindwa kubuni mbinu mpya ya mapambanoya kisiasa. “Kwa
ujumla wake Mh. Rais Magufuli anakubalika kwa asilimia 89% huku
akiwapiku Edward Lowassa na Mh. Jakaya Kikwete ambao wao wamegawana
zilizobaki, Mh. Kikwete asilimia 7% na Mh. Edward Lowassa akiwa na
asilimia 4%.
Dotto Nyirenda, Mwanadiplomasia, CZI.
Akizungumzia
mkutano mkuu maalum wa CCM, Mwanadiplomasia Dotto Nyirenda yeye
amewaasa wana CCM kutambua mambo 10 ambayo Rais Magufuli anatosha
kuyasimamia.
Aliyateja
mambo hayo kuwa ni pamoja na rasilimali watu, rasilimali ardhi, majengo
na viwanja, wanazuoni wa kila taaluma, wafanyabiashara ndogondogo
(machinga), wanayabiashara, wanachama wanaozidi milioni 9, Mashabiki
wake wanaozidi milioni 28.9, wakulima, wavuvi, na wafugaji, laini pamoja
na “utajiri” huo, CCM haiwezi kujiendesha na inategemea ruzuku kutoka
ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, pamoja na wafadhili ambao wengine
sio wasafi kwenye rekodi zao.
Imeandikwa na K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
Juma George Chikawe, Mtaalamu wa Teknohama CZI.


Blogger Comment
Facebook Comment