Mbio
za Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy
zimekisha baada ya mshambuliaji huyo kuongeza mkataba wa miaka minne
kuendelea kuichezea klabu yake hiyo na sasa Arsenal inaonekana kubadili
mwelekeo.
Akitoa
maoni yake baada ya Vardy kuongeza mkataba, kocha wa Arsenal alisema
wanaweza kutuma ofa ya kutaka kumsajili kiungo wa Leicester City, N’Golo
Kante lakini ni mapema kwa sasa kuzungumzia hilo.
“Nadhani Leicester wametoa suluhisho kuwa Vardy atasalia klabuni hapo. Tulikuwa tukimuhitaji lakini kwa sasa hakuna la zaidi,
Kuhusu
Kante Wenger alisema “Ni ngumu kwa sasa kuzungumza kuhusu hilo kwa
wakati huu, Kante yupo katika orodha ya wachezaji ambao wanahitajika
katika vilabu vingi, tutaona lipi litatokea kwa wiki mbili au tatu
zijazo,
“Kama
ukiuliza watu 100 mtaani kuwa wanahitaji Kate acheze timu ya taifa ya
Ufaransa, utapata watu wote wakitaka awepo amefanya kazi nzuri katika
mechi ambazo amecheza na hilo halinishangazi,” alisema Wenger.


Blogger Comment
Facebook Comment