Dr. Shein Aahidi Kutumbua Majipu ndani ya CCM

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewataka wanaCCM kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha chama na kuahidi kuyatumbua majipu hadi katika chama.

Dk Shein alisema kwa upande wa serikali kazi ya kuunda serikali inaendelea na kuwataka watendaji walioteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali kufanya kazi kwa maslahi ya taifa na wananchi wake.

Alisema mtendaji atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake katika sehemu za kazi ni bora akajiondoa kabisa hata kabla ya kusubiri kuondolewa. 

Kwa upande wa CCM, aliwataka watendaji kusimamia majukumu yao bila ya kusubiri kusimamiwa kwa ajili ya kuimarisha chama, kwani kazi hiyo ni ya kujitolea na waliopewa dhamana hizo wanatakiwa kulifahamu hilo na kujituma kwa kujenga chama imara.

“Wapo watendaji katika chama hawatekelezi na kusimamia majukumu yao vizuri na kama ndiyo majipu yenyewe basi tutayaondoa,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment