Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva amesema kumekuwa na upotoshaji kuhusu mchakato wa Katiba mpya ambao kwa sasa umefikia katika hatua ya Kura ya Maoni.
Lubuva amesema NEC iliusitisha ili kupisha Uchaguzi Mkuu mwaka jana.
Lubuva amesema NEC iliusitisha ili kupisha Uchaguzi Mkuu mwaka jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba amesema ingawa Rais John Magufuli wakati akizindua Bunge mwishoni mwa mwaka jana alitamka kutambua uwapo wa kiporo cha kukamilisha Katiba mpya, sasa anapaswa kuonyesha hatua za kukamilisha shughuli hiyo.
Hata hivyo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema NEC ndiyo inayotakiwa kusema ni lini mchakato wa Katiba utaendelea kwa sababu wao ndiyo waliousitisha.
“NEC wakisema, serikalini tutaendelea na maandalizi ya mchakato huo kwa yanayohusu upande wetu …hata tukisema kubadilisha sheria sasa na NEC hawajataja ni lini si zitapitwa na wakati tena? Amesema.



Blogger Comment
Facebook Comment