Kama mwanamke ambaye ndoa ilifungwa kiislamu anaolewa wakati wa kipindi cha eda hakijaisha basi ndoa hiyo itakuwa batili.
Lakini mfaruku hiyo ni pale iwapo mtalikiwa awe anafuata dini ya Kiislamu.
Kama atabadili dini baada ya kufiwa au kupewa talaka masharti ya eda
hayatambana na atakuwa huru kuolewa.
Aina za ufungaji ndoa na taratibu za kufuata
Taarifa ya nia ya kuoa
Kwanza
kama mwanamke na mwanamme wanataka kufunga ndoa ni wajibu taarifa ya
nia ya kufunga ndoa itolewe kwa mfungishaji ndoa siku 21 kabla ya
siku ya kufunga ndoa.
Taarifa hiyo ionyeshe mambo yafuatayo:-
(i) Majina kamili na umri wa wanaotaka kuoana.
(ii) Uthibitisho kwamba hakuna kipingamizi
dhidi ya hiyo ndoa wanayotarajia kufunga.
(iii) Majina kamili ya wazazi wao na sehemu wanakoishi.
(iv) Hadhi ya wafunga ndoa, yaani kama ni
mwanamke ifahamike kama hajaolewa,
ametalakiwa au ni mjane na mwanamme
pia anapaswa kama hajaoa, au ana mke au/wake wengine (hii ni kwa ndoa za
kiserikali na kiislamuu) au kama ametaliki.
(v)Kama muolewaji ana umri chini ya miaka 18, jina la mtu aliyetoa idhini ya yeye
kuolewa kama yupo ionyeshwe.
(vi) Kama ni ndoa ya kiserikali au kiislamuu
hapana budi kueleza kama ndoa ni ya wake
wengi au inatazamiwa kuwa ya wake wengi,
majina ya wake waliopo yatajwe.
Pia katika fungu hili kama mtu anataka ndoa iwe ya mke mmoja anapaswa kueleza.
Baada ya taarifa yenye maelezo haya kufikishwa kwa mfungishaji ndoa yeye anawajibika kutangaza hii nia ya kufunga ndoa.
Sababu ya kufanya hivyo ni ili kama kuna mwenye kipinganizi na ndoa hiyo atoe taarifa.
Matangazo haya hutolewa kama ndoa inatarajiwa kufungwa kidini, sehemu za ibada.
Kama ni ndoa ya kiserikali tangazo litabandikwa nje ya ofisi ya msajili wa Ndoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya.
Vipingamizi vya ndoa viko vya aina mbili, cha kwanza ni kile cha kisheria yaani
kama ndoa itakayofungwa itakuwa batili.
Kipingamizi
cha pili ni kama muoaji ana mke au wake wengine tayari, hivyo mke au
wake wanaweza kutoa kipingamizi kama uwezo wa muoaji kifedha ni mdogo
kiasi kwamba kuongeza mke mwingine kutazidisha shida.
Mfungishaji ndoa anapopokea taarifa ya kupinga ndoa isifungwe, ataipeleka taarifa hiyo kwenye Baraza la Usuluhishi la Ndoa.
Huko aliyewekewa kipingamizi na aliyeweka wataitwa na kila mmoja
atajieleza.
Baada ya kusikiliza pande zote Baraza
lina uwezo wa kuamua ndoa hiyo ifungwe au isifungwe na mfungishaji ndoa atafuata uamuzi wa Baraza.
Kama mtu atatoa kipingamizi cha uongo na ikithibitika hivyo, adhabu yake anaweza kufungwa kifungo kisichozidi miaka mitatu.
Baada ya kipengele hiki kutimizwa ndoa inaweza kufungwa.
Aina za ndoa
Kama tulivyosema awali kuna aina mbili za ndoa.
(a) Ndoa ya mke mmoja
Huu ni muungano unaoruhusu mwanamme kuoa si zaidi ya mke mmoja, mfano wa aina hii ya ndoa ni ndoa ya Kikiristo.
(b) Ndoa ya zaidi ya mke mmoja
Huu ni muungano unaoruhusu mwanamme kuoa mke zaidi ya mmoja, mfano wa aina hii ya ndoa ni ndoa za Kiislamu na ndoa za kimila.
Sheria ya ndoa inatambua aina tatu za ufungaji wa ndoa yaani kiserikali, kidini na kimila.


Blogger Comment
Facebook Comment