Polisi Jijini Mwanza Waua Jambazi Mmoja Usiku Huu.......Jambazi Mwingine Akimbia, Polisi Mmoja Ajeruhiwa


Polisi mkoani Mwanza wamemuua jambazi mmoja baada ya kujibizana kwa risasi mida  ya  saa 7 ( saba ) usiku 

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio, amesema katika tukio hilo, askari mmoja amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni na jambazi huyo aliyeuawa ambaye alikuwa na mwenzake anayedaiwa kukimbilia kwenye majabali ya mawe.

Amesema majibizano hayo yalianza saa 6.20 katika Mtaa wa Utemini, baada ya polisi waliokuwa doria kufuatilia nyendo za watu hao.

“Tulipokea taarifa kutoka kwa raia  wema kuwa katika eneo hilo kuna watu wanaowatilia shaka, ndipo askari wakaamua kuwafuatilia. " 

Hata hivyo, amesema wamefanikiwa kukamata bastola moja iliyokuwa ikitumiwa na jambazi huyo.

“Unasikia milio hiyo ya risasi, askari wanaendelea kumsaka huyo mmoja aliyejificha kwenye mawe, naimani tutampata tu na hatuondoki hapa mpaka tumtie mikononi,” alisema Msangi na kuongeza:

“Hawa ni majambazi sugu ambao walikuwa wakituhumiwa kufanya matukio ya uporaji na mauaji jijini hapa, tulikuwa tukiwasaka kwa muda mrefu.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment