Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta akimtoka mchezaji wa Misri jijini Dar es Salaam wakati wa kicheza kati ya timu ya Taifa Taifa Stars na Misri.

Na Zainab Nyamka, Blogu ya Jamii.
NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta amemuomba Nadir Haroub 'Canavaro'arejee kwenye kikosi cha Stars kwani bado ana uwezo wa kucheza na uwepo wake kwenye kikosi hicho ni muhimu ukizingatia uzoefu wa muda mrefu katika michuano mbalimbali ya kimataifa.
Samata amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mtanange wao dhid ya Misri uliomalizika kwa Taifa Stars kufungwa goli 2-0 na kufuta matumaini ya kufuzu michuano ya mataifa Afrika AFCON 2017 nchini Gabon.
Amesema uwezo wa kumshawishi mchezaji kurejea kwenye kikosi hicho ila Canavaro ni mtu mzima na ana maamuzi yake ya nini anachotaka kufanya ambacho kina faida kwake.
"Ninao uwezo wa kumshawishi mchezaji yoyote yule kurejea kwenye kikosi ila kila mmoja ana maamuzi yake na ukiangalia Canavaro ni mtu mzima na anajua nini anachofanya zaidi nachoweza kusema tunaomba aje kwenye timu kwanza ana uzoefu wa siku nyingi hasa michuano ya kimataifa,"amesema Samatta.
Canavaro aliamua kuachana na timu hiyo miezi sita iliyopita na ameweka wazi msimamo wake wa kutokucheza timu hiyo hata baada ya kuitwa tena na kocha mkuu wa timu hiyo, Charles Mkwasa.
Blogger Comment
Facebook Comment