Vitisho Kwa Njia ya Simu Vyamfikisha Mahakamani.

Mkazi wa Kijiji cha Misasi Mariamu Nestory (20) amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kujibu shtaka la kutoa lugha ya vitisho kwa njia ya simu.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Doroth Mgenyi alidai kuwa Mei 2  saa 8:15 mchana,  mshtakiwa  huyo kwa kutumia simu  aliandika ujumbe wa vitisho kwa Diana Kabula kinyume cha sheria ya makosa ya mtandao kifungu 18 (1) ya mwaka 2015.

Alinukuu ujumbe huyo akidai:  “Ujiandae siku utakayoingia anga zangu, sali sala ya mwisho, ulisikia kisa cha Sengerema ndivyo nitakavyokufanya... ikishindikana kukuua kwa mikono yangu nitakuroga uwe kichaa.” 

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana shtaka.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment