Baada
ya tetesi za muda mrefu za Manchester United kumtaka kiungo mshambuiaji
wa Borussia Dortmund, Henrikh Mkhitaryan hatimaye Dortmund imetoa
taarifa kuhusu mchezaji huyo kuwa atajiunga Man United kwa kitita cha
Pauni Milioni 26.
Katika
taarifa ambayo imetolewa na Dortmund imeeleza kuwa wamechukua uamuzi wa
kumruhusu Mkhitaryan kujiunga Man United kwani akisalia katika timu
hiyo 2017 ataondoka bure kwakuwa mkataba wake utakuwa umemalizika.
“Manchester
United walituletea ofa kubwa lakini tuliikataa na tunatambua mchezaji
atakuwa huru kuondoka 2017,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Dortmund,
Hans-Joachim Watzke katika taarifa iliyotolewa na klabu na kuongeza.
“Borussia Dortmund inamtakia kila la heri Henrikh Mkhitaryan kwa msimu ujao kwa Ligi Kuu ya Uingereza na UEFA Europa League”
Mkhitaryan
alitua Dortmund mwaka 2013 akitokea Shakhtar Donetsk kwa kitita cha
Pauni Milioni 27.5 kipindi hicho Dortmund ikinolewa na Jurgen Klopp
ambaye kwa sasa anainoa Liverpool.


Blogger Comment
Facebook Comment