July
28 2016 Chama cha mapinduzi (CCM) kikiongozwa na msemaji wake
Christopher Ole Sendeka kimekutana na waandishi wa habari Dar es salaam
na kuzungumzia hatua iliyotangazwa na chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA kufanya maandamano ya nchi nzima.
"Jana tarehe 27/7/2016 chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), walitoa kauli iliyojaa uongo mwingi za kibabaishaji na kuthibitisha ukweli kuwa kwa hakika kutokana na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli wapinzani wamekosa ajenda.
"Katika
uongo na uzushi walioutangaza, CHADEMA wanasema wameamua kufanya
mikutano na maandamano nchi nzima, kimsingi hoja walizozitumia zimejaa
upotoshaji na uongo uliokithiri. Ifahamike kuwa serikali haijazuia
mikutano kwenye majimbo yao.
"Wabunge
wako huru kufanya shughuli zao na tumeona baadhi ya wabunge wakifanya
shughuli zao majimboni bila shida wakiwemo hao wa upinzani.
"Ni vizuri tukakumbuka matukio kwenye operesheni kama hizi yaliyopoteza maisha ya vijana wetu na matokeo ya kila operation" –Ole Sendeka






Blogger Comment
Facebook Comment