Mapigano yaripotiwa Sudan Kusini




Sudan Kusini
Mapigano makali yameripotiwa katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba.
Mapigano hayo yameripotiwa katika maeneo tofauti lakini haijabainika ni nani anayetekeleza mashambulio.
Tayari rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amewaagiza raia kuwa watulivu huku ufyatulianaji risasi ukiendelea katika mji huo mkuu, kulingana na chombo cha habari cha reuters.
Siku ya Alhamisi wanajeshi watano waliuawa na wapiganaji walio watiifu kwa makamu wa rais Riek Machar.
Kuna serikali ya umoja baada ya kukamilika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua miaka miwili.BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment