HATIMAYE
ile safari ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba iliyoendeshwa na Kampuni
ya Global Publishers, jana Alhamisi ilifika tamati baada ya kudumu kwa
takribani miezi sita, ambapo kulifanyika kwa droo kubwa katika Viwanja
wa Zakhem, Mbagala jijini Dar na mshindi kupatikana.
Nelly
Mwangosi mkazi wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni mama wa nyumbani mwenye
watoto wawili ndiye aliibuka mshindi wa nyumba hiyo ya kisasa iliyopo
Salasala jijini Dar yenye samani zote za ndani mpya kabisa na mshindi
huyo anatarajia kukabidhiwa mali yake hivi karibuni.
Mara
baada ya kupigiwa simu kutaarifiwa kuwa yeye ndiye mshindi, mama huyo
alisema “Yesu wangu!! Nimefurahi kuona kuwa nimeibuka mshindi, najisikia
raha sana, nawaombea Global kwa Mwenyezi Mungu.” Shughuli hiyo
ilitarajiwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
ambaye hata hivyo aliwakilishwa na Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah
Chaurembo ambaye ndiye aliyesoma jina la mshindi huyo.
Bahati
nasibu hiyo ya Shinda Nyumba ilisimamiwa na Afisa Mwandamizi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo akisoma jina la mshindi wa nyumba, ambaye ni Nelly Mwangosi kutoka Iringa.
Mbali
na mshindi wa nyumba, pia kulikuwa na zawadi ndogondogo zilizotolewa
kwa washindi wengine. Washindi hao ni Peter Mihayo, Issa Leon Mallya,
Frank Ndambo (wote Bed sheets), Mahmoud Mhina alishinda vyombo vya
nyumbani (Dinner set) huku Method Kunambi na Halima wakishinda simu ya
kisasa (Smartphone).
Wengine
ni ving’amuzi vitano vya TING ambapo washindi wake ni Godfrey Mkombo wa
Morogoro, Wilbert John mkazi wa Kinondoni, Dar, Baltazar Mrosso kutoka
Moshi, Magreth Ndambo wa Tabata, Dar sambamba na Jane Liwinga mkazi wa
Dodoma. Pia Hawa Maulidi mkazi wa Mlole, Kigoma alishinda Bed Sheet,
huku Helman Haule wa Dodoma akijinyakulia Dinner Set.
Bahati
nasibu hiyo ya Shinda Nyumba ilikuwa ikiendeshwa na kampuni hii kupitia
kwa magazeti yake ya Risasi, Amani, Uwazi, Championi, Ijumaa Wikienda
yanayopatikana kwa shilingi 500 huku lile la Ijumaa linalotoka Ijumaa
likiuzwa kwa shilingi 1,000 pekee.
MC Chaku akimpigia simu mshindi wa nyumba, Nelly Mwangosi kutoka Iringa.
Wakati
mchakato wa kuelekea kumpata mshindi huyo jana ukiendelea, wananchi
wengi walionekana kufurahishwa na kilichokuwa kikitokea huku wakisema
kuwa Global imeweka historia kwa kuwa tukio kama hilo ni nadra kutokea
kwa shilingi 500 kumpatia nyumba mtu tena ndani ya Dar es Salaam.
Aidha,
kuna wale ambao walionekana kuwa na furaha kupitiliza na kujikuta
wakitoa machozi ya furaha kwa kuona nyumba hiyo imeenda kwa mama wa
nyumbani ambaye hana kazi. Katika maelezo yake Nelly alisema kwa sasa
ana watoto wawili lakini alikuwa nao wanne, wawili walishatangulia mbele
ya haki.
Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo akizibwa macho ili akachague kuponi ya mshindi.
Abdallah Chaurembo akiwa na kuponi ya mshindi wa nyumba.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiwashukuru Watanzania wote walioshiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.
Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers, Oscar Ndauka akichukua zawadi ya Dinner Set tayari kumkabidhi mshindi.
Mahmoud Mhina akitokomea na zawadi yake ya Dinner Set.
Mmoja
wa Ma MC wa kilele cha bahati nasibu ya Shinda Nyumba, Kelvin Shayo
(kushoto) akiwa na mmoja wa wasomaji wa magazeti ya Global aliyekuwa
akisoma jina la mshindi wa zawadi ya Bedsheet.
Mshindi wa simu ya kisasa (Smartphone), Method Kunambi (kulia) akipokea zawadi yake.
Zoezi la kusoma majina ya washindi wa zawadi ndogondogo likiendelea.


Blogger Comment
Facebook Comment