Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara kuwa
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).
Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara
anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro
ambaye muda wake umemalizika.
Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Julai, 2016.
Kwa mujibu wa sheria ya Mamlaka ya
usafiri wa anga ya mwaka 1977 Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya
Mamlaka hiyo huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambapo Mwenyekiti akitoka Tanzania Bara, Makamu Mwenyekiti hutoka
Tanzania Zanzibar na kinyume chake.
Wakati huo huo, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempandisha
cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kedmon Andrew Mnubi kuwa Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).
SACP Kedmon Andrew Mnubi pamoja na
makamishna wengine 59 ambao Rais Magufuli amewapandisha vyeo kuanzia
tarehe 16 Julai, 2016 watakula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma
kesho jumatatu tarehe 18 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam saa tatu
asubuhi.
Rais Magufuli atakuwepo wakati
Makamishna wote 60 wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi
ambalo litaendeshwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
Wote wakaohudhuria tukio hili wanatakiwa
kufika Ikulu kabla ya saa mbili na nusu asubuhi na wataingia kupitia
lango kuu la mashariki (lango la baharini).
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
17 Julai, 2016
Blogger Comment
Facebook Comment