Wasomi nchini wamesema iwapo Waziri Mkuu mstaafu, Frederick
Sumaye atakuwa mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, atasaidia kukijenga
chama hicho cha upinzani nchini, kuanzia ngazi ya chini.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti walisema jana kuwa Sumaye ambaye juzi alirejesha
fomu ya kuwania nafasi hiyo, katika ofisi za kanda hiyo Dar es Salaam,
akitumia uzoefu alionao kiuongozi, atakuwa msaada kwa chama hicho.
Walisema uamuzi huo umeonyesha kuwa hakuhamia Chadema kwa masilahi
binafsi. Profesa George Shumbusho wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema:
“Inaonekana (Sumaye) ana lengo la kusaidia upinzani ukue. Kwa mchango na
uzoefu wake serikalini ataisaidia sana Chadema maana chama lazima kiwe
na nguvu kuanzia ngazi ya chini.”
Sumaye ndiye Waziri Mkuu pekee katika
historia ya Tanzania kushika wadhifa huo kwa miaka 10 baada ya kuwa
msaidizi wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kati ya mwaka 1995 hadi 2005.
Agosti mwaka jana, Sumaye aliyekuwa kete muhimu katika kampeni za
aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa kutokana kuikosoa
Serikali na kuwataka Watanzania kutoichagua CCM, alitangaza kuachana na
chama hicho tawala na kujiunga na upinzani.
Shumbusho alisema ameonyesha kuwa yeye siyo aina ya wastaafu
wanaopenda sifa na hakwenda kusaka ulaji Chadema huku akibainisha nchi
ikiwa na upinzani imara, chama kilichopo madarakani hugangamala.
Blogger Comment
Facebook Comment