Kutokana na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini, leo August 24 2016 Jeshi la Polisi limepiga marufuku mikutano yote ya kivyama ndani na nje ili kuzuia machafuko ya amani yanayoendelea kujitokeza katika kipindi hiki.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu amesema Jeshi la polisi halikuzuia mikutano ya ndani ya siasa kwasababu lilikuwa linaamini ni mikutano iliyokuwa ikizungumzia maendeleo ya wananchi
Amesema Jeshi hilo limebaini kwamba mikutano hiyo imekuwa ikitumika kuchochea wananchi na kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na kufanya mapambano na jeshi la polisi
"Kwasababu hiyo basi,kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini linapiga marufuku mikutano yote ya ndani" amesema IGP Ernest Mangu
0 comments :
Post a Comment