Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa 2016/2017 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), beki wa kati wa Manchester United, Daley Blind amefunguka kuhusu nafasi yake katika kikosi cha kocha Mourinho.
Blind alisema ugumu huo unatokana na ujio wa kocha mpya katika klabu hiyo ambaye ana mfumo wake na ujio wa wachezaji wapya ambapo kwa upande wa nafasi ambazo anacheza yeye tayari amesajiliwa Eric Bailly na hivi karibuni Paul Pogba anataraji kuwasili.
Alisema ili anajiamini kuwa ana kiwango kizuri lakini anahitajii kufanya mazoezi zaidi ili kufanya vizuri zaidi pindi anapopatiwa nafasi ya kucheza.
“Ninajiamini na uwezo wangu na ninatakiwa kuonyesha zaidi na zaidi, nadhani kwa michezo ya kuajiandaa na msimu mpya mpaka sasa nimefanya kazi kubwa na nitaendelea kuongeza juhudi,
“Bado hajasema jambo kuhusu mimi na hata watu wengine, nahitaji kufanya mazoezi kwa bidii na kupata nafasi katika timu. Nafikiri kila mwalimu ana mawazo yake, huyu ni kocha mkubwa na mipango yake na kama timu tunajifunza mengi,” alisema Blind.