Ndugu JPM, milimoni? Dodoma, mji mzuri wenye mengi mazuri.
Ndoto
za Dodoma za Baba wa Taifa, kijana wa Mwitongo Juliasi Nyerere, si
ndoto tena bali uhalisia Safari imeanza, na mabegi tayari tumebeba.
Tatizo,
uzuri wa Dodoma umeingia shubiri Si kwa kasi hii Kubwa, si kupinga
fikra zako sahihi kama Mwenyekiti wa Chama na AmiriJeshi Mkuu Bali ni
vipele vilivyogeuka majipu kwenye mahusiano Kumbuka zile semina na
mikutano ya nenda lala siku mbili Dodoma urudi Ijumaa ilikuwa ni homa
kali kwenye mahusiano.
Ndugu
JPM, Mahusiano ndio msingi wa nguvukazi ya taifa. Wafanyakazi wanapokua
wametulizwa kwenye mahusiano, huweza kufanya kazi kwa bidii na kasi ya
kustaajabisha.
Yaani
ukisema hapa kazi tu, wala hawashangai. Nasema kutoka moyoni, maana
msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Safari ya Dodoma ni maumivu kwa
mahusiano machanga na yale makongwe
Inawezekana
kujipanga kwenda baadae kidogo BABA?. Tunaomba nafasi ya kupanga
utaratibu wa mahusiano, yaani kujua tunayaweka-wekaje. Sijui kama unajua
ndugu JPM, Kwa
tamko lako tu kwamba asiyetaka safari ya Dodoma, atafute ajira mbadala,
uhusiano, uchumba, ndoa zote ni sawa na talaka tatu, hakuna rejea.
Yaani ni kama vile ng’ombe wa masikini hazai. Unajua mahusiano mengi yalikuwa yanawezeshwa na vile vinanihii, maana misongo ya utumbuaji majipu ni balaa
Wala havikuwa vinachochea yale mengine. Wahusika wa yale mambo wanajulikana .. Tuwatafute hao
Sasa marufuku imetangazwa kwa vilinda mahusiano na ndoa
Kwa wanawake na wanaume, mambo ni ngumu zaidi hasa wale walio safarini kuelekea Idodomya
Mkuu,
tembeza huruma yako, mioyo ya watu ipate kupumua maana ingekuwa
uhamisho wa mtu mmoja mmoja ni msiba binafsi, huu wa jumla ni kilio
nyumba kwa nyumba mtaani
tunakuja Dodoma
yaiya
0 comments :
Post a Comment