Tangawizi ni kiungo muhimu katika chakula ambacho asili yake ni katika maeneo ya kitropiki ya kusini mwa bara la Asia, kiungo hichi pia kinadhaniwa kuwa kina asili ya ukanda wa nchi ya India
Tangawizi iliweza kufika Afrika kama tokeo la biashara ya nafaka na mazao baina ya bara la Asia na Afrika enzi za ukoloni, japokuwa zipo taarifa za kihistoria zinazoeleza kuwa Tangawizi ilikuwepo Afrika ila watu hawakuwa na ufahamu nayo wala matumizi.
Kiungo hichi muhimu kina matumizi mbalimbali yanayotegemea kusudio la mtu mwenyewe kwani Tangawizi hutumika kutengenezea siki au sherry, wengine hutengeneza vitafunwa kama biskuti /kuki(bites/biscuits,cookies) au kupikwa kama kiungo katika vyakula vingi. Lakini pia tangawizi inaweza kutengeneza pipi, mvinyo na vingine vingi.
Wengine hupenda kutumia kiungo hichi katika upishi wa chai na utengenezaji wa sharubati/juisi (juice)
Lakini pia katika sekta ya afya Tangawizi ina historia ndefu ya matumizi kwa kupunguza matatizo ya utumbo kama vile kichefuchefu, kupoteza hamu ya kula, ugonjwa mwendo na maumivu.
Ginger_Tea_Have_Any_Bad_Side_Effects
Tangawizi ilianza kutumika mashariki ya mbali, kama vile China na India wakitumia kwa kutibu maradhi mbali mbali. Katika hili zao la tangawizi kuna vyanzo vya:
-Magnesium
-Manganese
-Potasium
-Copper
-Vitamini B6
katika mwili wa binaadamu wataalam na wagunduzi wanasema kuwa Tangawizi ni  tiba tosha kwa magonjwa  mengi
-Husaidia kutibu magonjwa ya ngozi
-Husaidia kupunguza kama si kuondoa kichefuchefu ni nzuri haswa kwa wale wanawake wenye mimba changa ambao husumbuliwa kutapika.
-Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia maumivu makali kupata ahueni, pia husaidia kusambaza damu kwenye mwili kwa haraka zaidi.
-Husaidia msago wa chakula kwa haraka zaidi kwa kuchanganya na tindikali tumboni.
-Husaidia kwa wale wanaosafiri baharini ikiwa na machafuko kuzuia kutapika,kwa kutumia nusu saa kabla ya kusafiri na boti.
-Husaidia kupigana na kukinga kansaa ya kizazi.
-Tangawizi husaidia kupunguza maumivu mwilini
-Husaidia kutoganda kwa damu mwilini
-Wataalamu wamegundua tangawizi ni dawa tosha ya presha kuliko kitunguu swaumu.
-Husaidia kuponya mafua kwani chai ya tangawizi ni salama