Kuweni makini na matapeli wa ardhi Dodoma - Mabula

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amewataka wananchi mkoani Dodoma kuwa makini kabla ya kununua ardhi kwa kuhakikisha wamepita kwenye ofisi za serikali ili kuepuka utapeli.

Akizungumza katika kipindi cha NIPASHE kinachorushwa na Radio One, Mabula amesema kutokana na serikali kutangaza kuhamia Dodoma, ardhi imeanza kuuzwa sana hivyo wananchi wawe makini kwa kuzingatia taratibu na wasiishie kwenye ofisi ndogo za mitaa kwani kama watakuwa hawana ramani wanaweza kununua eneo ambalo limepangiwa shughuli nyingine.

“Wananchi waende Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ndiyo itawapa ramani za viwanja vya maeneo na shughuli ambazo zinaonekana kwenye ramani tofauti na hapo mtu anaweza kununua ardhi ambayo ni halali na kuepuka ghadhabu ambayo inaweza kuja kutokea baadaye” Amesema Mabula.

Aidha hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu CDA, Pascas Muragili alisema tayari mamlaka hiyo imeshafanya kazi ya kuupanga mji huo hivyo wananchi watakaotoka katika maeneo mbalimbali wawe makini wasije kuuziwa ardhi kinyemela jambo ambalo litawaletea usumbufu na kupoteza fedha zao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment