Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati) akikata utepe kuzindua
rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es
salaam huku akiambatana na Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo na
Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha.
Mkuu
wa Bidhaa na Huduma za Mitandao, Silvest Arumasi akimpa maelekezo Mkuu
wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mara baada ya kufungua rasmi tawi
la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es salaam.
Pembeni yake ni Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo.
Mkuu
wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha akiongea machache
wakati wa ufunguzi rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach
jana jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa
benki ya First National kwa kuendelea kufungua matawi yake pembezoni mwa
mji wa Dar es Salaam ambapo alisema ni jambo la faraja sana pale mteja
anapofuatwa alipo na si kila siku kukimbilia kufungua benki katikati ya
mji. Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili toka kulia) akiwa na
Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo ( kwanza kulia) pamoja na
viongozi wa benki ya First National. Kulia ni Mkuu wa Huduma za
Rejareja, Francois Botha na Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Mitandao,
Silvest Arumasi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiongea machache na mmoja ya kiongozi wa Benki hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya First National na wageni waliohudhuria uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akifanyiwa mahojiano na waandishi
wa habari. -- Ikiwa ni sehemu ya mkakati wake kuwafikishia Watanzania
wengi zaidi huduma za kibenki na kukuza uchumi, First National Bank
imefungua tawi Mbezi Beach na kufanya idadi ya mtandao wa matawi yake
kufikia nane.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa tawi hilo jipya lililopo Shamo Towers Mbezi, mkuu
wa kitengo cha wateja wa rejareja wa benki hiyo Francois Botha amesema
leo kwamba ufunguzi wa tawi hilo ni sehemu ya mkakati wa kufikisha
huduma za kibenki katika maeneo yote muhimu ya jiji la Dar es salaam na
nchi nzima na kuinua uchumi wa Watanzania kupitia huduma mbalimbali kama
mikopo ya nyumba na mikopo kwa wafanyabiashara wadogo,wa kati na
wakubwa.
“Mara
kwa mara tunafikiria mbinu mpya za kutuwezesha kutoa huduma inayowapa
unafuu wateja wetu kwa kupeleka huduma hiyo karibu na makazi pamoja na
biashara zao. Tawi hili litarahisisha huduma kwa wateja wetu wanaoishii
Mbezi na maeneo ya jirani ambayo yana biashara nyingi zinazokua kwa
kasi,” alisema Botha.
Mkuu
wa kitengo cha bidhaa na huduma za kidigitali wa First National Bank,
Silvest Arumasi, alisema kuwa kutokana na ukuaji wa kasi wa jiji la Dar
es salaam benki hiyo imeona umuhimu wa kuhakikisha huduma za kisasa za
kibenki zinawafikia watu wengi zaidi.
“Tunataka
kuhakikisha tunatoa mchango muhimu katika kuendeleza sekta ya fedha
nchini na tumepanga kuendelea kuanzisha huduma mpya zenye ubunifu na za
kitaalamu hapa nchini,” alisema Arumasi. Tawi hilo lililofunguliwa Mbezi
Beach Shamo Towers litatoa huduma za kibenki mahususi kukidhi mahitaji
ya watumiaji huduma pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo.
0 comments :
Post a Comment