Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC kimelaani vikali maneno yanayotolewa na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali maneno ambayo wamedai yanazidi kuchochea chuki na uhasama miongoni mwa watanzania na kujenga hofu kubwa katika nchi.
Hayo yemeelezwa ikiwa nchini Tanzania kuna vugu vugu kubwa la kisiasa huku kambi mbili za kisiasa ambazo ni chama kikuu cha upinzani na serikali wakijibishana kwa kauli mbalimbali kuhusu maandamano ambayo yamepangwa kufanyika na chama kikuu cha Upinzani CHADEMA wiki ijayo.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa kumekuwa na kauli kali na za kutisha zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa na Viongozi wa serikali ambazo zisipozuiliwa zinaweza kulifarakanisha taifa na kujenga chuki kubwa.
Amesema kuwa kumwekuwepo na hali ya kutishiana baina ya viongozi wa vyama,viongozi wa serikali,,jeshi la polisi na raia kwa kauli hizo zenye kuleta hofu kwa raia wanachama na wasio wanachama wa vyama vya siasa hasa kutokana na watanzania kutokuwa na uzoefu wa lugha hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC IMELD LULU URIO(kulia) akisisitiza Jambo wakati wa mkutao huo wa wanahabari |
Akitolea mfano wa Lugha ambazo zimekuwa zikitolewa siku za hivi karibuni ni pamoja na maneno kama Udicteta Uchwara,UKUTA, Kuwashughulikia, Viberiti vya Gesi, Sijaribiwi, Tumejiandaa kufa,Kuvunjwa Miguu,Kuwekwa ndani na maneno mengine ambayo wanadai hayastahili kutumika katika nchi ambayo inatajwa kuwa kisiwa cha amani Africa.
Aidha Mama Hellen ameongeza kuwa siku za hivi karibuni tumeshudia jeshi la polisi nchini ambalo jukumu lake ni la kikatiba na kisheria ni kulinda Raia na mali zao likijipambanua kama jeshi la kupambana na wananchi na kufanya mazoezi na majaribio ya vifaa vya jeshi hilo kwenye mitaa na makazi ya watu wakilipua milipuko bila sababu za msingi hali ambayo imewajaza hofu wananchi ambao hawaelewi kinachoendelea.
Katika hatua nyingine LHRC wamemshauri Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli Kujenga utamaduni wa kutoa kauli zinazofwata misingi ya haki za binadamu na uheshimuji wa sheria.wameeleza kuwa Kauli mbalimbali zinazotolewa na Rais zimekuwa zikikiuka sheria na misingi ya haki za Binadamu nchini Jambo ambalo linaweza kusababisha makubwa katika Taifa.
“Mfano akiwa Ziarani mkoani singida alituoa Tamko la kuzuia mikutano na shughuli za kisiasa hadi mwaka 2020 jambo ambalo ni kinyume na sheria ya vyama vya siasa na katiba ya nchi”amesema Hellen.
Pamoja na Ombi hilo kwa Mh Rais amesema kuwa wapo viongozi wengine wa serikali ambao nao wameingia katika mkumbo huo wa kutumia Lugha mbaya na kuvunja katiba na sheria kama Waziri mkuu alivyopiga marufuku mikutano ya siasa pamoja na kukanusha kauli hiyo,huku pia wakuu wa mikoa pamoja na viongozi mbalimbali wa jeshi la polisi wamekuwa wakitoa matamko yenye makatazo ya mikutano na mikusanyiko ya kisiasa jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Kuhusu mauaji yaliyotokea juzi Mbagala Jijini Dar es salaam ya askari polisi wane wa jeshi la polisi kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kwa masikitiko makubwa wamelaani vikali mauaji hayo na kutoa pole kwa kamanda wa Jeshi la polisi Nchini Ispekta Jenerali wa polisi Ernest Mangu kwa tukio Hilo.
LHRC wamelitaka jeshi la polisi nchini kuzidi kuimarisha dhana ya polisi Jamii iliyoasisiwa miaka michache Iliyopita ili kusaidia katika kuimarisha ulinzi wa Raia na mali zao.
0 comments :
Post a Comment