Makonda awafungukia walionukuu kauli yake vibaya


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amefafanua juu ya kauli yake aliyoitoa hivi karibuni ambayo imekuwa ikinukuliwa vibaya na vyombo vya habari ikiwemo gazeti la leo la Mwananchi.

Kwenye ukurasa wa tatu, gazeti hilo limeandika habari yenye kichwa kinachosomeka, “Makonda ataka wahalifu wagongwe, wapigwe.”

Akiongea na Clouds 360 ya Clouds FM, Makonda amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanapenda kuwagombanisha wananchi na viongozi wao kutokana na kauli wanazozinukuu kutoka kwao.

“Unajua kuna baadhi ya wenzetu wana agenda zao tofauti na agenda ya kujenga taifa, watu ambao wangependa kuwatengenezea mazingira wananchi wasielewane na viongozi wao,” amesema Makonda.

“Kwa sababu ukiangalia hii stori ilivyoandikwa kuna kitu kimewekwa ambacho hakipo kabisa lakini kimewekwa kwa tafsiri ya kumsaidia mwenye kusudi la kufikisha ujumbe tofauti na ule uliotolewa,” ameongeza.

Aidha Makonda ameendelea kwa kufafanua kauli yake hiyo iliyonukuliwa vibaya kwa kudai kuwa, “unapokuwa msituni ni sawa na mapambano lazima upambane kwa kuwalinda polisi wako, majambazi siyo watu wazuri kutokana na tukio lililotokea la kuuawa kwa polisi wanne hivi karibuni.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment