Zikiwa
zimesalia siku tatu kabla ya kuanza kwa michezo mikubwa ya Olimpiki
ambayo kwa mwaka 2016 inafanyika nchini Brazil maandalizi ya sherehe za
ufunguzi tayari yameanza kufanyika.
Mwanamitindo
wa Brazil, Gisele Bundchen anataraji kupamba sherehe za ufunguzi ambazo
zitafanyika katika uwanja wa Maracana uliopo Rio de Janeiro ufunguzi
ambao utahudhuriwa na wageni mbalimbali ambao wamealikwa kushuhudia ufunguzi huo.
Aidha
watu milioni 900 wanatarajiwa kutazama sherehe hizo kupitia tv na
mitandao mbalimbali sehemu zote duniani ambayo itakuwa live kuonyesha
sherehe za ufunguzi wa Olimpiki 2016.
Mashindano ya mwaka huu yanataraji kuanza Agosti, 5 na kumalizika Agosti, 21, Mo Blog tumekuwekea picha 15 kuaona jinsi maandalizi ya sherehe za ufunguzi yanavyofanyika.
Mwanamitindo, Gisele Bundchen atatumika kupamba ufunguzi wa michezo ya Olimpiki 2016.
Blogger Comment
Facebook Comment