Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Mhe, Nape Moses Nnauye, ametahadharisha vyombo vya habari katika maudhui yao wakati wa uandishi wa habari pamoja na utangazaji wa habari hususani pale wanapo enda kinyume na sheria za nchi.
Amevitaka vyombo vya habari kufwata kanuni na taratibu zilizo wekwa na taasisi za habari, huku akikazi katika kuhakikisha wanaepuka mahudhui yenye uchochezi au hali ya uvunjifu wa amani katika nchi yetu.
Mhe. Nape ametangaza rasmi kuanzia leo tarehe 29/8/2016 kuzifungia kwa muda Radio 5 ilioko jijini Arusha, pamoja na Radio Magic iliopo jijini Dar es salaam, kutokana na kuwa na habari za uchochezi katika vipindi vyao.
“Leo tarehe 29/8/2016 nazifungia rasmi Radio 5 ya Arusha na Radio Magic ya Dar es salaam kwa kurusha vipindi vyenye maudhui ya uchochoze wa kuhatarisha Amani ya nchi”, alisema Nape
Pia ameitaka kamati ya maudhui iliopo TCRA kuwaita wahusika hao na kuzungumza nao kwa kina ili kuweza kuleta ushauri kwangu tujue nini cha kufanya kutokana na makosa hayo.
Mhe. Waziri alidai kwamba katika “kipindi cha matukio” kilicho rushwa na Radio 5 pamoja na kipindi cha “tunapaka rangi” cha Radio magic, vilikua vimejikita katika kuongea maneno ya uchochezi ambayo yange weza kuvunja Amani katika nchi yetu.
Aidha Nape amewapongeza baadhi ya vyombo vya habari kwa kanzi nzuri wanazo fanya na kuwataka kuendelea hivyo kwani lengo ni kujenga na sio kubomoa.
“kama serikali tunatambua mchango mkubwa wa tasnia hii katika kuleta habari, Amani na maendeleo kwa jamii hivyo hatuna budi kutoa pongezi kwa wote wanao fanya vizuri”, alisema waziri Nape.
0 comments :
Post a Comment