Tokeo la picha la mrema
Pamoja na kazi ambayo inafanywa naPolisi Jamii ya kuhakikisha kunakuwa na usalama katika maeneo mbalimbali nchini, Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini, Augustino Mrema amemtaka Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Naibu Kamishna Mohamed Mpinga kuwaondoa Polisi Jamii katika maeneo yote waliyopo.
Mrema amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa Polisi Jamii wamekuwa wakiwakamata wahanga wa madawa ya kulevya wa nia ya kutaka kupewa rushwa na ndio kufanya kazi ambayo wamekusudiwa kuifanya.
Mrema amesema Polisi Jamii wamekuwa wakiwatesa wahanga wa madawa ya kulevya na hata alipofatilia kufahamu uhalali wa watu hao kufanya vitendo hivyo aliona wanafanya makosa na hivyo kummwambia IGP Mangu ndani ya siku saba watu hao watolewe ili wahanga wasipate mateso.
“Hawa Polisi Jamii na Polisi Shirikishi hawana nia ya kukomesha matumizi ya madawa ila tu wanataka rushwa na mimi nimemtaka Kamanda Mpinga awatoe hao wanaojiita Polisi Jamii na Polisi Shirikishi,
“Na hili jambo nimekuwa nikipigana na RC na DC hawa wahanga kukamatwa na Polisi Jamii kwanza vijana ambao hawajaanza kutumia tiba hawawakiwi kupelekwa mahabusu, wao wanatakiwa kwenda hospitali kupatiwa tiba,” alisema Mrema.
Pia Mrema alitumia nafasi hiyo kutuma ujumbe kwa mahakimu nchini akiwataka kuwa makini na hukumu ambazo wanatoa kwa watumiaji wa madawa ya kulevya kwani wakiwahukumu kwenda gerezani inakuwa ni ngumu kupata tiba hivyo ni vyema kama wakiwa wanahukumiwa vifungo vya nje ili wapate tiba.
“Mahakimu mnisikilize la sivyo nitawachongea kwa Magufuli, mnawafunga watumiaji wa madawa ili iweje na katiba inaruhusu wanaweza kufungwa kifungo cha nje … mtumiaji akiwa gerezani ni ngumu sana kupata tiba na naambiwa gharama ni mara 10 zaidi kumhudumia mtumiaji aliye gerezani kuliko aliye huru,
“Hawa atuamiaji wasipelekwe magarezani muwapelekea katika vituo vya tiba vya Muhimbili, Temeke na Mwananyaala ili waanze kupata tiba, kila siku asubuhi saa 12 wanatakiwa kumeza dawa ili wapone na wao wanaiomba serikali iwape kazi hata kama ni mashamba ili wakalime,” alisema Mrema.
Aidha Mrema aliwataka vijana kuwa makini katika kipindi hiki ambacho hivi karibuni Chadema inataraji kufanya maandamano kwani kama watakubali kutumika wanaweza kujiingiza katika hatari na kuchukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola.