Hatimaye ndoto ya watanzania kumwona mtanzania mwenzao, Mbwana Ally Samatta akicheza katika mashindano yanayoshika nafasi ya pili kwa ukubwa barani Ulaya ambayo yanahusisha vilabu ya Europa League sasa imetimia.
Hilo limekamilika baada ya Genk kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya NK Lokomotiva na hivyo kuwa na ushindi wa jumla wa goli 4 kwa 2, ushindi ambao umeiwezesha Genk kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Vilabu Ulaya (UEFA Europa League).
Katika michezo yote miwili ambayo Genk imefunga magoli mawili, Samatta amefunga magoli mawili na mwenzake Leon Bailey akifunga mawili.
Droo ya makundi inataraji kupangwa leo Ijumaa na michezo ya kwanza inataraji kuchezwa Septemba, 15.