Tamko la pamoja limesomwa katika sherehe zilizofanyika mji mkuu wa Cuba huko Havana
Serikali ya Colombia na kundi la waasi la Farc wamesaini mkataba wa amani kusitisha mgogoro uliopo zaidi ya miongo mitano.
Wananchi wa Colombia wakifurahia baada ya makubaliano hayo
Pande zote mbili zimekubaliana kusaidia jamii, kuwapa haki zao waathirika wa mgogoro huo na kuleta amani.
Tamko la pamoja limesomwa katika sherehe zilizofanyika mji mkuu wa Cuba huko Havana,ambapo makubaliano hayo ya amani yalianzishwa karibu mika 4 iliyopita.
Mgogoro huo umesababisha vifo vya watu zaidi ya laki mbili na kuaawacha zaidi ya milioni bila ya makazi huko colombia.
Muda wa makubaliano wa mkataba huo bado unahitajika kuwekwa na wananchi wa Colombia kupitia kura ya pamoja itakayofanyika mwezi oktoba.
Farc wamekuwa wakipigana na serikali tokea mwaka 1964
Chanzo:BBC
0 comments :
Post a Comment