Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015/2016, Yanga leo Jumapili ya Agosti, 28 wamechez mchezo wao wa kwanza wa VPL kwa msimu wa 2016/2017 dhidi ya African Lyon mchezo ambao umepigwa katika uwanja wa taifa.
Mchezo huo umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3-0, magoli ya Yanga yakifungwa na Deus Kaseke katika dakika ya 18, goli la pili likifungwa na Simon Msuva dakika ya 59 na goli la tatu likifungwa na Juma Mahadhi katika dakika ya 90+2.
Baada ya kuondoka na alama zote tatu za mchezo huo, mchezo unaofuatia kwa Yanga unataraji kuwa dhidi ya JKT Ruvu, mchezo unaotaraji kupigwa Jumatano katika uwanja wa Taifa.
Matokeo mengine ya michezo ya leo ni, Toto Africans amefungwa goli 1-0 na Mbeya City, goli la Mbeya City likifungwa na Haruna Shamte katika dakika ya 6 ya mchezo huo.
0 comments :
Post a Comment