Kijana Saidi Juma Mnyambi (26) aliyeng’atwa 1/3 ya ulimi wake wakati wakinyonyana ndimi na mwanamke mmoja,ameingiwa na hofu kubwa kuwa mchumba wake anaweza kumwacha/kumtema,kutokana na kitendo hicho.
Saidi mkazi wa Unyankhae kata ya Mandewa Manispaa ya Singida, ameyasema hayo juzi wakati alipotembelewa hospitalini na mwandishi wa habari hii.
Alisema hofu hiyo na wasi wasi huo mkubwa alionao, unachangiwa kwa kiasi kikubwa na kitendo hicho kuwa gumzo kubwa ndani na nje ya manispaa ys Singida.
“Kabla ya tukio hilo,uchumba wangu ulikuwa unaendelea vizuri na mambo yalikuwa wanakwenda mwishoni mwishoni, kuelekea kufunga ndoa .Lakini sasa nina hofu mwenzangu anaweza akapotoshwa na mambo yakaharibika. Nikitoa hospitalini hapa baada ya kupona, nitalifuatilia jambo hili kwa ukaribu zaidi,ili kuwaka mambo sawa,” alisema Saidi huku akitambasamu.
Kuhusu ulimi wake uliong’atwa, Saidi alisema unaendelea vizuri na sasa anaongea vizuri kama ilivyo kwa binadamu ambaye ulimi wake ni kamili. Maumivu nayo yamepungua.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida,Peter Kakamba,amekiri kuwa wanamshikilia mwanamke huyo (jina hajalitaja) aliyemng’ata ulimi Saidi, na wanaendelea na upelelezi.Baada ya kukamilika kwa upelelezi huo, sheria zitachukua mkondo wake.
Aidha, alisema bado mkuu wa upelelezi (RCO) makosa ya jinai,anakamilisha uchunguzi .Hata hivyo, alidai taarifa za awali ya tukio hilo la majeruhi huyo Saidi, ni tofauti na hali halisi ilivyokuwa.
“Baada ya kumpata mwanamke anayetuhumiwa kumng’ata ulimi Saidi,zimepatikana taarifa mpya.Waandishi wa habari kuweni na subira tutawapatia taarifa zenye mashiko wakati wo wote kuanzia sasa”,alisema Kamanda Kakamba.
Na Nathaniel Limu, Singida