Jaji nchini Uganda atishia kuwaachilia huru washukiwa wa ugaidi


media
Washukiwa wa ugaidi waliokamatwa nchini Uganda
Jaji wa Mahakama maalum inayoshughulikia kesi za uhalifu wa Kimataifa katika Mahakama kuu jijini Kampala nchini Uganda, ametishia kuwaachilia huru washukiwa wa ugaidi kutoka kundi la Al Shabab nchini Somalia.
Jaji Elizabeth Nyahamya amesema washukiwa hao nane wataachiliwa huru ikiwa serikali itashindwa kuanza kesi dhidi yao kama ilivyoahidi.
Washukiwa hao wamekuwa wakifika Mahakamani mara kwa mara lakini hawafunguliwi mashtaka, hali ambayo imewakera mawakili na washukiwa wenyewe.
Kiongozi wa mashtaka Rachael Bikoli anayeiwakilisha serikali katika kesi hii, ameiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe 15 mwezi Desemba atakapokuwa tayari kuwafungulia mashitaka washukiwa hao.
“Umesema kwa mdomo wako mwenyewe kuwa, kesi hii itaanza tarehe 15 mwezi Desemba, sitaahirisha tena kesi hii, ikiwa haitaanza, sitakuwa na lingine bali kuwaachilia huru washukiwa hawa kwa sababu hakuna ushahidi,” alisema Jaji Nyahamya.
Washukiwa hao raia wa Somalia wametajwa kuwa; Mohamed Abdulkadir Hirsi anayejulikana kwa jina maarufuku kama Mohamed Abdul Aziz Adan, Abdi Abdullahi Bootan, Hassan Abduwali Mohamoud, Mohamed Ahmed Gele, Yusuf Osman Hussein, Abdi Ali, Abdul Kadir Mohamed Mohamud Sandir na Mohamad Yusuf Farah.
Washukiwa hao walikamatwa mwaka 2014 na wamekuwa wakizuiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka ya ugaidi kwa muda huo wote. RFI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment