Baada ya miezi 10 tangu aliyekuwa rais wa Chama cha Soka Ulaya (UEFA) asimamishwe kazi kutokana na kuhusiswa na uhujumu wa fedha za FIFA kiasi cha pesa za Swiss Milioni mbili, UEFA imepata rais mpya, Aleksander Ceferin.
Aleksander Ceferin amekuwa rais mpya wa UEFA baada ya kumshinda mpinzani wake katika kinyang`anyiro cha nafasi hiyo, Michael va Praag.
Ceferin ambaye ni rais wa Chama cha Soka cha Slovenia, ameshinda uchaguzi huo kwa kupata kura 42 kati ya 55 zilizopingwa na wanachama wa UEFA.
Akizungumza kuhusu ushindi wa nafasi hiyo, alisema “Nchi yangu ni ndogo na nzuri ya Slovenia inajivunia sana kupata nafasi hii na naamini siku moja kila mmoja atajivunia mimi,
“Baadhi ya watu wanasema siwezi kuwa kiongozi, sababu naonekana mdogo na sina uzoefu wa kutosha kuwa rais wa UEFA, unaweza kusema mimi bado mdogo na sina uzoefu lakini kiukweli huu ni ukosefu wa heshima, baaada ya mwaka wa siku 365, nitakuwa nimefanya zaidi ya hapa,” alisema Ceferin.


0 comments :
Post a Comment